#Business

RUTO AZINDUA DHAMANA YA TAIFA

Rais William Ruto amezindua dhamana ya taifa katika soko la hisa la Nairobi ili kufadhili ujenzi wa Uwanja wa Michezo wa Talanta unaojengwa na kampuni ya Kichina.

Rais Ruto amesema kuzinduliwa kwa dhamana hiyo kutakusanya zaidi ya shilingi bilioni 44 za Kenya (sawa ana dola za Kimarekani milioni 340.6), ambayo ni mafanikio makubwa yanayothibitisha imani kwa Kenya kwenye masoko ya fedha.

Vile vile amesema mapato yanayotokana na dhamana hiyo yatasaidia ujenzi wa Uwanja wa Talanta wenye uwezo wa kuchukua watu 60,000, ambao utaongeza sifa ya Kenya kimataifa kama ngome ya michezo.

Uwanja huo utakaokuwa wa viwango vya FIFA, unajengwa na kampuni ya China Roads and Bridges, unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa 2025, na utatumika kwenye sherehe za ufunguzi, ufungaji, na mechi za Kombe la Mataifa ya Afrika la 2027 (AFCON), umati mkubwa ukitarajiwa na hivyo kuimarisha shughuli za kibiashara.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

RUTO AZINDUA DHAMANA YA TAIFA

UHAMISHO WA LIGI KUU YA UINGEREZA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *