MADAI YA OMTATAH YAIBUA UTATA BUSIA
Afisi ya gavana wa Busia Paul Otuoma imekanusha madai ya kutumia visivyo shilingi bilioni 5 za bajeti ya mwaka wa kifedha wa 2022-23 jinsi ilivyoibuliwa na seneta wa kaunti hiyo Okiya Omtatah.
Kupitia taarifa kwa vyombo vya habari, afisi hiyo imemtaka Omtatah kuomba msamaha kutokana na kauli zake la sivyo achukuliwe hatua za kisheria.
Hata hivyo kulingana na seneta huyo, afisi ya gavana Otuoma ilipenyeza matumizi ya ziada kwenye bajeti hiyo licha ya kutokuwepo kwenye bajeti ya awali.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































