#Local News

UPINZANI WAPIGANIA MCHELE

Mrengo wa upinzani umeikosoa serikali ya Kenya Kwanza kwa madai ya kuwasaliiti wakulima nchini, kufuatia tangazo la serikali kwamba inalenga kuagiza tani elfu 500 za mchele kutoka mataifa ya nje.

Ukiongozwa na kinara wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka, upinzani umesema mpango huo utafanikisha ufujaji wa fedha za umma mbali na kulemaza shughuli za kilimo nchini, kauli iliyosisistizwa na baadhi ya viongozi wa Kenya Kwanza akiwemo gavana wa Kirinyaga Anne Waiguru.

Hata hivyo, serikali imeahidi kununua mchele ulio kwenye maghala.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

UPINZANI WAPIGANIA MCHELE

KARO VYUONI YAPUNGUZWA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *