#Business

TAARIFA YA EAC KUHUSU TAHARUKI

Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) imesisitiza tena ahadi yake kuendeleza mchakato wa mafungamano ya kikanda baada ya Tanzania kupiga marufuku wageni kuendesha biashara ndogo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na katibu mkuu wa EAC Veronica Nduva, nchi wanachama zinatakiwa kufuata itifaki ya Soko la Pamoja la Jumuiya hiyo, ambayo inahimiza usafirishaji huru wa bidhaa, huduma na watu katika kanda hiyo.

Taarifa hiyo imesisitiza nchi wanachama zinatakiwa kuepuka kubadilisha au kuzuia sekta na biashara huria, huku ikinukuu kifungu cha 5 cha ratiba ya ahadi ya mpango wa soko la pamoja la EAC kuhusu utoaji huru wa huduma.

Jumuiya ya EAC imehimiza nchi zote wanachama kutekeleza wajibu wao wa mkataba kulinda ukamilifu wa soko moja la kikanda.

Imetayarishwa na Maureen Amwai

TAARIFA YA EAC KUHUSU TAHARUKI

“KAULI ZA WIZI’ ZAKOSOLEWA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *