MFUMO WA MISHAHARA WAENDELEA KUMPORA MKENYA, RIPOTI
Serikali inapoteza mamilioni ya pesa kila mwezi kutokana na kasoro zilizo kwenye mfumo wa mishahara ya sekta ya umma.
Haya ni kulingana na ripoti ya mkaguzi wa hesabu za serikali Nancy Gathungu, ikionyesha uwepo wa wafanyakazi hewa, malipo ya kupita kiasi na tofauti ya kiasi cha mishahara kwa wafanyakazi walio katika ngazi sawa kwenye sekta mbali mbali.
Aidha, ripoti hiyo imesema baadhi ya wafanyakazi halali wa serikali hulipwa kwa kuchelewa kinyume na sheria.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 




















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































