MAREJEO YA FUJO
Watu kadhaa wakiwemo wanahabari wanaendelea kuuguza majeraha baada ya kujeruhiwa hapo jana kwenye makabiliano kati ya wafuasi wa kiongozi wa chama cha DCP Rigathi Gachagua na wahuni waliokuwa wamejihami waliojaribu kuvuruga msafara wa Gachagua kutoka uwanja wa ndege JKIA.
Kundi hilo la wahuni lilirushia mawe msafara huo na kuwajeruhi wafuasi wa DCP mbali na kuharibu magari, muda mfupi baada ya msafara huo kuondoka katika uwanja wa JKIA
Gachagua alikuwa akirejea nchini kutoka Marekani.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































