#Business

KENYA, MAREKANI KUANZA MAZUNGUMZO KUHUSU MKATABA MPYA WA BIASHARA AGOA IKIKAMILIKA.


Kenya na Marekani zinatazamiwa kuanza mazungumzo kuhusu makubaliano mapya ya kibiashara huku muda wa mwisho wa Septemba 30 wa Sheria ya Ukuaji na Fursa Afrika (AGOA) ukikaribia.

Waziri wa Biashara Lee Kinyanjui alisema mpango huo ni muhimu ili kupata ufikiaji unaoendelea bila ushuru kwa bidhaa za Kenya na kuvutia uwekezaji mpya, kufuatia kukwama kwa mazungumzo ya STIP chini ya utawala wa Joe Biden.

 Wizara ya Biashara ilitaja mkutano na Mwakilishi wa Biashara wa Marekani Jamieson Greer mjini Washington kuwa hatua muhimu, ingawa mwelekeo wa mazungumzo bado hauko wazi chini ya sera ya Rais Donald Trump ya “Marekani Kwanza”.

Imetayarishwa na Maureen Amwayi

KENYA, MAREKANI KUANZA MAZUNGUMZO KUHUSU MKATABA MPYA WA BIASHARA AGOA IKIKAMILIKA.

JOBO WAPIGWA CHOBO NA MUSINGU

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *