WIZARA YAFICHUA ULAGHAI KUPITIA SHA
Wizara ya afya imeimarisha juhudi zake za kukabili ulaghai wa hospitali kuhusiana na malipo ya bima ya SHA, ikisema imezuia ulipaji wa shilingi bilioni 10.6 zilizokuwa zikitumwa kwa hospitali kadhaa kupitia njia za udanganyifu.
Kulingana na waziri wa afya Aden Duale, vituo vya afya 45 vinavyodaiwa kutumia udanganyifu kuilaghai bima hiyo vimefungwa kwa kukosa kufuata mwongozo wa matibabu.
Duale amesema kaunti ya Mandera inaongoza kwa visa vya udanganyifu chini ya bima hiyo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































