TAHARUKI NAIROBI KUHUSU HOJA YA KUMBANDUA SAKAJA
Wawakilishi wadi katika bunge la kaunti ya Nairobi wamepanga kuwasilisha bungeni hoja ya kumtimua kutoka afisini gavana Johnson Sakaja na naibu wake Njoroge Muchiri hii leo.
Wawakilishi wadi wapatao 90 wameripotiwa kutia Saini hoja hiyo na hivyo kuzidi kiwango hitajika cha 41 ili kuwasilisha hoja hiyo bungeni.
Miongoni mwa tuhuma zaidi ya 20 wanazoibua ni madai kwamba majukumu ya bunge la kaunti hiyo yamepuuzwa na serikali tendaji.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































