MARUFUKU YA UKATAJI MITI YAONDOLEWA
Ni afueni kwa wafanyabiashara katika sekta ya mbao baada ya rais William Ruto kuondoa marufuku ya ukataji miti katika misitu ya umma nchini, hatua anayosema itabuni nafasi za ajira mbali ya kusitisha uagizaji wa fenicha.
Rais aliondoa marufuku hiyo alipokuwa katika eneo la Elburgon kaunti ya Nakuru, na kutamatisha marufuku ya miaka 6 iliyowekwa ili kulinda misitu.
Aidha, rais ametangaza kuongeza ujenzi wa barabara ya Nakuru-Mau Summit hadi Malaba.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































