#Football #Sports

IVORY COAST WAMJUMUISHA ZAHA KIKOSINI

Mabingwa watetezi wa dimba la taifa bingwa barani Afrika Ivory Coast wamemrejesha kikosini wing’a wa zamani wa Crystal Palace Wilfried Zaha mwenye umri wa miaka 33, wanapojiandaa kutetea taji hilo katika mashindano ya mwaka huu baadaye mwezi huu nchini Morocco.

Zaha ambaye kwa sasa anawajibikia klabu ya Charlotte nchini Marekani, alijumuishwa kwenye kikosi cha wachezaji 26 ambacho kitamenyana na Mozambique, Cameroon na Gabon katika Group F ya kipute hicho.

Alitemwa na kikosi hicho katika mashindano ya mwaka 2023 yaliyochezwa mwaka jana nyumbani, ambapo The Elephants waliwanyuga Nigeria 2-1 kwenye fainali na kutawazwa mabingwa.

Kocha wa timu ya taifa ya Ivory Coast Emerse Fae, amesema wanahitaji wachezaji wenye uzoefu.

Zaha ambaye aliichezea Manchester United mechi 4 pekee katika kipindi cha miaka 2 kabla ya kuuzwa Palace, aliichezea timu ya taifa ya Uingereza mara 2 kabla ya kubadilisha uraia.

Kiungo wa kati anayecheza nchini Slovenia Jean-Michael Seri pia amejumuishwa.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

IVORY COAST WAMJUMUISHA ZAHA KIKOSINI

FKF YAINGIA MOU KUINUA SOKA YA VIJANA

IVORY COAST WAMJUMUISHA ZAHA KIKOSINI

LIVERPOOL WAONYESHA MWANGA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *