LSK KUPINGA UAMUZI WA MAHAKAMA
Chama cha mawakili nchini LSK kimetishia kupinga uamuzi wa mahakama ya Nakuru kuwazuia mawakili wa kibinafsi kuwakilisha idara za serikali mahakamani, kikisema uamuzi huo ni vita dhidi ya taaluma ya uanasheria.
Rais wa LSK Faith Odhiambo, amekosoa uamuzi huo anaosema ni utumizi mbaya wa mamlaka ya idara ya mahakama, wakitaka agizo hilo libatilishwe.
Hata hivyo, waliowasilisha kesi iliyosababisha uamuzi huo, wanasema hatua hiyo itapunguza ubadhirifu wa fedha za umma.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































