#Football #Sports

CARRICK AHIMIZA UDHABITI UNITED

Meneja mshikilizi wa klabu ya Manchester United Michael Carrick, amewataka wachezaji wake kuonyesha viwango sawa walivyoonyesha kwenye ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya majirani zao Manchester City Jumamosi, mechi ambayo iliashiria mwanzo mpya Old Trafford.

United walichochewa na mabadiliko katika uongozi, mabao ya Brian Mbeumo na Patrick Dorgu yakitia breki kwa juhudi za City kunyakua taji la ligi kuu ya Uingereza, EPL.

United pia walishuhhudia mabao 3 yakifutiliwa mbali kutokana na ofsaidi, mbali na kunyimwa mabao zaidi na ubora wa kipa Gianluigi Donnarumma.

Carrick aliyetueliwa kuiongoza klabu hiyo aliyeichezea miaka ya zamani, aliwapongeza vijana wake na kusema ndoto yao itaafikiwa tu iwapo watadumisha viwango hivyo.

Katika matokeo mengine, Arsenal waliongeza mwanya wa pointi licha ya sare ya kutofungana dhidi ya Nottingham Forest, wakipata afueni zaidi baada ya washindani wao wa karibu Aston Villa kupokezwa kichapo cha bao 1-0 na Everton.

Kwenye msimamo wa ligi, Arsenal wanaongoza wakiwa na pointi 50, City na Villa wakifuata kwa pointi 43, Liverpool wanashikilia nafasi ya 4 kwa pointi 36, moja mbele ya United. 

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

CARRICK AHIMIZA UDHABITI UNITED

MMUST RUGBY WAPATA USHINDI ADIMU

CARRICK AHIMIZA UDHABITI UNITED

UKAME WAATHIRI WANYAMAPORI LAMU

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *