#International

KAGAME AITAKA RWANDA ‘KUJITEGEMEA’

Rais wa Rwanda Paul Kagame, amewahimiza wananchi wake kuimarisha mikakati ya kujitegemea huku wito wa kutaka Amerika iiwekee vikwazo nchini hiyo ukiongezeka.

Rwanda imekuwa ikikosolewa na jamii ya kimataifa kuhusiana uungwaji wake mkono wa kundi la wapiganaji la M23 Mashariki wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC, ingawa Rwanda imekuwa ikisema kuhusika kwake nchini humo ni kuzuia kuibuka kwa waasi waliosalia wakati wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda.

Akizungumza katika hafla moja, Kagame amesema taifa linajizatiti kujitegemea, ili kuwa huru kutoka kwa wale ambao wanaweza kusitisha msaada wao wakati wowote.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

KAGAME AITAKA RWANDA ‘KUJITEGEMEA’

RUTO ATETEA MIRADI YAKE

KAGAME AITAKA RWANDA ‘KUJITEGEMEA’

LIONESSES WAREJEA NCHINI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *