POLISI WAKAMATA WASHUKIWA SABA MUMIAS MASHARIKI
Maafisa wa polisi katika eneo bunge la Mumias Mashariki wamewakamata washukiwa saba wa uhalifu wanaodaiwa kuhusishwa na kundi la Jeshi Jinga ambalo limekuwa likiwahangaisha wakaazi wa eneo hilo.
Kamanda wa polisi wa eneo hilo, Doris Chemos, amethibitisha kuwa washukiwa hao walikamatwa baada ya kuvamia waombolezaji katika eneo la Mwitoti, ambako walishambulia watu kwa kuwakata na kuharibu mali.
Aidha, Chemos amewarai wazazi kuwafuatilia kwa karibu watoto wao na kuchunguza mienendo yao, akionya kuwa yeyote atakayenaswa akijihusisha na uhalifu atachukuliwa hatua kali za kisheria.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































