#Football #Sports

HARAMBEE STARLETS WANOLEWA MAKALI KABLA YA WAFCON 2026

Timu ya taifa ya soka ya wanawake, Harambee Starlets, imeongeza makali ya maandalizi yake kuelekea Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake, WAFCON 2026, kupitia kambi ndogo ya ndani inayolenga kuchunguza vipaji vipya na kuimarisha kikosi.

Kambi hiyo inayoendelea imewakutanisha wachezaji waliobobea kutoka ligi za humu nchini, na kuwapa fursa ya kupata uzoefu wa kuchezea timu ya taifa chini ya kocha mkuu Beldine Odemba.

Kocha Odemba amesema soka la wanawake nchini linaendelea kupiga hatua, hususan katika Ligi Kuu ya Wanawake, akisisitiza kuwa kambi kama hizi ni muhimu si tu kwa maandalizi ya mashindano yajayo bali pia kwa kujenga falsafa ya muda mrefu ya uchezaji wa timu ya taifa.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *