VIONGOZI WA TAITA TAVETA WALAANI UKEKETAJI
Viongozi kutoka kaunti ya Taita Taveta wanasema kuna haja ya juhudi zaidi hapa nchini ili kumaliza ukeketaji.
Wakizungumza katika kaunti hiyo viongozi hao Wamesema visa vya ukeketaji vimekuwa vikiendelezwa hasa katika maeneo ya mipakani mwa Kenya na Tanzania.
Aidha, viongozi hao wamesema ukeketaji unafanywa sio tu kwa wasichana wa shule za msingi na upili, bali pia kwa watoto wadogo, jambo linalotia wasiwasi mkubwa kijamii na kiafya.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































