OBURU AONYA VIONGOZI WA ODM KUHUSU NIDHAMU
Kiongozi wa chama cha ODM, Oburu Oginga, amewakosoa vikali maafisa wakuu wa chama wanaodaiwa kukiuka maamuzi ya vyombo muhimu vya chama, akionya kuwa ukosefu wa nidhamu miongoni mwa uongozi unatishia mshikamano wa ODM.
Akihutubia kikao cha Kamati Kuu ya Kitaifa (NEC) kilichofanyika Mombasa, Oburu amesema baadhi ya wanachama wa Kamati ya Utendaji na Kamati Kuu wamekuwa wakitoa kauli hadharani zinazokinzana na maazimio yaliyopitishwa na vyombo halali vya chama.
Ingawa amekiri kuwa wanachama wa kawaida wana haki ya kidemokrasia ya kutoa maoni binafsi, Oburu amesisitiza kuwa viongozi wa ngazi za juu wanawajibika kuheshimu maamuzi ya pamoja na kuzingatia uwajibikaji wa pamoja katika uongozi wa chama.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































