RISING STARLETS YAPANIA HATUA NYINGINE DHIDI YA TANZANIA
Rising Starlets wana matumaini ya kufuzu raundi inayofuata ya kufuzu Kombe la Dunia la FIFA kwa Wanawake chini ya miaka 20 wanapojiandaa kuvaana na Tanzania katika mechi ya marudiano itakayochezwa Jumamosi jijini Dar es Salaam. Kenya inaongoza kwa bao 1-0 kutoka mkondo wa kwanza uliochezwa Februari 7jijini Nairobi.
Bao hilo la ushindi lilifungwa dakika za mwisho na Elizabeth Mideva, lakini kikosi kinasisitiza kuwa bado kazi haijakamilika. Timu ya taifa inasema ipo makini na imejikita kwenye maandalizi kamili ikizingatia kuwa dakika 90 pekee ndizo zinazitenganisha na kufuzu raundi ya nne na ya mwisho.
Kiungo Sunira Manda amesema benchi la ufundi na wachezaji wametumia siku chache zilizopita kurekebisha makosa yaliyojitokeza katika mechi ya kwanza. Ameongeza kuwa timu iko tayari kupambana na kulinda ushindi wao ugenini.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































