#Local News

SERIKALI YAHAKIKISHIA FAMILIA YA SHANTEL HAKI

Katibu Mkuu wa Wizara ya Jinsia na Uwezeshaji, Anne Wang’ombe, amewahakikishia wakazi kuwa haki itatendeka haraka kufuatia mauaji ya kinyama ya msichana wa miaka tisa, Shantel Waruguru, aliyedaiwa kuuawa na jamaa yake mwishoni mwa wiki iliyopita.

Wang’ombe ametoa kauli hiyo alipowatembelea wanafamilia wa marehemu katika kijiji cha Kianjogu, eneobunge la Mathira, ambako huzuni na hasira vilitawala huku jamaa na majirani wakikusanyika kuomboleza kifo cha mtoto huyo aliyeaga dunia katika mazingira ya kusikitisha.

Aidha, Wang’ombe amesisitiza kuwa serikali itaongeza juhudi na mikakati ya kukabiliana na visa vinavyoongezeka vya ukatili dhidi ya watoto.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *