#Local News

UPINZANI KUONGOZA MAANDAMANO YA WATU 100,000 NAIROBI

Viongozi wa upinzani nchini wametangaza kuongoza maandamano makubwa jijini Nairobi Ijumaa wiki hii kushinikiza kuwajibishwa kwa maafisa wa polisi wanaoaminika kuvuruga ibada iliyokuwa ikihudhuriwa na aliyekuwa naibu Rais Rigathi Gachagua mwezi jana kaunti ya Nyeri, baada ya juhudi zao kukutana na Inspekta mkuu wa polisi Douglas Kanja kufeli hapo jana.

Wakizungumza kwenye mkutano uliosambaratishwa na vitoza machozi eneo la Nyama Kima jijini Nairobi, viongozi hao akiwemo Gachagua na Kalonzo Musyoka wa Wiper, wamemtaka Waziri wa usalama wa kitaifa Kipchumba Murkomen, katibu wake mkuu Raymond Omollo pamoja na Kanja kujiuzulu kutokana na kuvuruguwa mara kwa mara kwa mikutano ya kisiasa.

Kulingana nao, idara ya polisi imepoteza uhuru wake kisheria.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *