#Football #Sports

DROO YA FA CUP 5TH ROUND

Droo ya raundi ya 5 ya dimba la FA Cup nchini Uingereza ilikamilika hapo jana, huku zawadi ya klabu ya Mansfield ya League One kuibandua Burnley ya ligi kuu, EPL, na kutinga awamu ya 5 ya FA baada ya miaka 50 ikiwa ni kukutanishwa na viongozi wa EPL Arsenal katika uwanja wa One Call.

Manchester City, ambao wameshinda taji hilo mara 7, mara ya mwisho ikiwa ni mwaka 2023, watahitaji kufanya walichofanya katika awamu ya nusu fainali ya dimba la Carabao iwapo watahitaji kusalia kwenye mkondo wa kushinda taji hilo kwa mara ya 8, baada ya kukutanishwa tena na Newcastle United.

Baada ya Brentford kutamatisha safari ya Macclesfield hapo jana waliowabandua mabingwa watetezi Crystal Palace, watamenya na West Ham kwenye debi la London katika uwanja wa London Stadium.

Na wakiwa wametinga awamu ya raundi ya 5 kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 29 kwa kuwachabanga Ipswich Town, Wrexham watamenyana bingwa mara 8 Chelsea ugani Racecourse Ground, huku bingwa wa mwaka 2022 Liverpool, akikutanishwa na Wolves wanaokabiliwa na hatari ya kushushwa daraja.

Kukamilisha ratiba ya raundi ya 5, Fulham watakuwa wenyeji wa Southampton, mshindi kati ya Bristol City apambane na Sunderland, naye Daniel Farke aiongoze Leeds United nyumbani dhidi ya mwajiri wake wa zamani Norwich City.

Mechi hizo zitasakatwa wikendi ya tarehe 6 mwezi ujao.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

DROO YA FA CUP 5TH ROUND

MIKAKATI YA RBA YA KULINDA PENISHENI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *