MURKOMEN AMJIBU VIKALI GACHAGUA
Waziri wa Usalama wa Ndani Kipchumba Murkomen amemjibu kwa ukali aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua, akimtuhumu kwa siasa za kugawa wananchi kwa misingi ya kikabila na siasa za kiwango cha chini, huku akionya kuwa hatanyamaza tena.
Akizungumza mjini Naivasha Murkomen amesema baadhi ya viongozi wa kisiasa wamejikita katika mashambulizi ya kibinafsi badala ya kuwasilisha sera mbadala, hasa katika masuala ya usalama.
Waziri huyo amesisitiza kuwa mjadala wa kitaifa unapaswa kujikita katika sera na suluhu za changamoto zinazowakabili wananchi, badala ya siasa za lawama na migawanyiko.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































