#Football #Sports

PEREIRA AANZA KWA KISHINDO FOREST IKIICHANA FENERBAHÇE

Kocha mkuu wa Nottingham Forest Vitor Pereira alianza kwa kishindo katika klabu hiyo kufuatia ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Fenerbahçe katika mkondo wa kwanza wa mwondoano wa dimba la Europa League jana usiku, nao Stuttgart wakiilaza Celtic mbao 4-1.

Pereira aliteuliwa kuwa mkufunzi wa 4 wa Forest msimu huu baada ya kukubali kutia Saini mkataba wa miezi 18 kuchukua mahala pa Sean Dyche aliyetimuliwa Jumapili iliyopita.

Alitangaza ujio wake kwa ushindi huo na kubadili mkondo wa matokeo ya Forest ambao wamekuwa katika hali duni, mabao hayo yakifungwa na Murillo, Igor Jesus na Morgan Gibbs-White.

Ushindi huo unawaweka katika hali nzuri ya kufuzu Raundi ya 16, watakapoialika Fenerbahçe katika mkondo wa mwisho Alhamisi wiki ijayo.

Katika jiji la Glasgow, kip awa Celtic Kasper Schmeichel alifanya makosa mawili hatari, na kuiacha klabu ya Martin O’Neil ikikadiria hasara katika mechi ya 1000 ya mkufunzi huyo.

O’Neil aliywaongoza Celtic kunaykua mataji 7 kati yam waka 2000-2005, alipokezwa kichapo cha 2 katika mechi 19 msimu huu.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

PEREIRA AANZA KWA KISHINDO FOREST IKIICHANA FENERBAHÇE

PETER WANYAMA AKUBALI MATOKEO LSK

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *