UPINZANI WAKEJELI KAULI ZA RUTO
Muungano wa upinzani umejitetea dhidi ya kauli za Rais William Ruto kwamba hauna ajenda yoyote ya maendeleo, badala yake muungano huo ukimkejeli rais kwamba rekodi aliyo nayo ni ukiukaji wa haki za kibinadamu na utawala wa sheria.
Viongozi wa muungano huo akiwemo Kalonzo Musyoka wa Wiper, Rigathi Gachagua wa DCP na naibu kinara wa Jubilee Fred Matiang’i, wamekariri kuwa ajenda yao ni kuwaondoa mamlakani viongozi wasio na uwezo wa kulinda mali ya umma.
Wamekariri kulinda kura zao wakati wa uchaguzi mkuu ujao.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































