#Local News

UDA MBELE KWENYE CHAGUZI ZOTE NDOGO

Chama cha UDA kimeratibiwa kunyakua nyadhifa zote za ubunge na uwakilishi wadi katika maeneo manne kulikofanyika uchaguzi mdogo hapo jana, wagombeaji wa nyadhifa hizo kwa tiketi ya UDA wakiongoza kulingana na matokeo ya awali.

Katika wadhifa wa ubunge eneo la Isiolo South, Tubi Mohammed Tubi aliyekuwa akiwania na dadake kumrithi baba yao, yuko mbele tayari huku wafuasi wake wakianza kusherehekea kabla yake kutangazwa mshindi.

Tayari Peterson Njiru wa UDA ametangazwa kuwa mshindi katika wadi ya Muminji, naye Dancun Muratia akiongoza katika wadi ya Evurore eneo bunge la Mbeere North, naye Elphas Shalako wa UDA akiongoza katika wadi ya West Kabras.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

UDA MBELE KWENYE CHAGUZI ZOTE NDOGO

NAIBU GAVANA WA HOMA BAY AJIUZULU

UDA MBELE KWENYE CHAGUZI ZOTE NDOGO

JUHUDI ZA INGWE KUNYAKUA TAJI ZAPATA PIGO

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *