NTSA KUTUMIA KAMERA MAALUM KUDUMISHA SHERIA BARABARANI
Rais William Ruto ameiagiza Mamlaka ya Kitaifa ya Uchukuzi na Usalama (NTSA), pamoja na Wizara ya Uchukuzi, kutekeleza mifumo ya kutumia kamera maalum za trafiki kuwanasa wanaovunja sheria katika barabara mbalimbali nchini.
Mpango huo unalenga kuimarisha usalama barabarani, kuboresha usimamizi wa trafiki, na kuimarisha utekelezaji wa kanuni za trafiki nchini kote.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































