#Football #Sports

FA CUP: SOUTHAMPTON KUKUTANA NA MANCHESTER CITY NUSU FAINALI

Southampton watakutana na Manchester City katika nusu fainali ya Kombe la FA uwanjani Wembley baada ya ushindi wao wa kushangaza dhidi ya vinara wa Ligi Kuu, Arsenal.

Southampton, wanaoshiriki Ligi ya Daraja la Pili, waliwashinda Arsenal mabao 2-1 katika robo fainali iliyochezwa St Mary’s Jumamosi, huku City wakiwachapa Liverpool mabao 4-0 kufuzu kwa mara ya nane mfululizo.

Timu ya kocha Pep Guardiola inalenga kufika fainali kwa mara ya nne mfululizo, huku Southampton wakitarajia kurudia historia ya ushindi wao wa kushangaza wa fainali ya mwaka 1976 dhidi ya Manchester United.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *