SIFUNA ALIOMBA TENA JOPO KUMWOKOA
Katibu mkuu wa chama cha ODM na ambaye pia ni seneta wa Nairobi Edwin Sifuna, amewasilisha tena ombi kwa jopo la kutatua migogoro ya kisiasa akitaka kufutiliwa mbali kwa uamuzi wa kamati kuu ya chama cha ODM kumtimua kutoka wadhifa wa katibu mkuu.
Kupitia kwa mawakili wake, Sifuna ameorodhesha ombi hilo kama dharura, akitaka kusitishwa kwa hatua zote za kinidhamu kuchukuliwa dhidi yake, kufuatia agizo la ODM kumtaka aeleze ni kwanini asitimuliwe.
Aidha, ameitaka afisi ya msajili wa vyama vya kisiasa kuzuiwa kuchapisha kutimuliwa kwake kwenye gazeti rasmi la serikali.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































