JEPCHIRCHIR AJIONDOA MBIO ZA LONDON
Bingwa wa dunia wa mbio za marathon Peres Jepchirchir amejiondoa katika mashindano ya London Marathon yanayotarajiwa kufanyika Aprili 26 kutokana na majeraha aliyopata mwezi Desemba.
Kujiondoa kwake kunafuatia pia hatua ya Sifan Hassan ambaye naye amejiondoa, hali inayopunguza ushindani mkali uliotarajiwa katika mbio hizo.
Waandaaji wamesema Jepchirchir amekuwa akisumbuliwa na jeraha tangu alipochuana katika mbio za Valencia, ambapo alimaliza wa pili nyuma ya Joyciline Jepkosgei.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































