#Rugby #Sports

SHUJAA YAJIANDAA KWA HONG KONG 7S

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya raga ya wachezaji saba Kevin Wambua ameongeza kasi ya maandalizi kuelekea mashindano ya Hong Kong 7s yatakayofanyika Aprili 17 hadi 19.

Mashindano hayo ni sehemu ya mfululizo wa Mashindano ya dunia ya HSBC na yanachukuliwa kama hatua muhimu kwa Kenya kurejea katika kiwango cha juu cha raga ya kimataifa ya wachezaji saba.

Wambua amebaki na kikosi kilichofanya vizuri katika SVNS 2 ambapo Shujaa walimaliza nafasi ya pili, akilenga kuimarisha uthabiti wa timu kuelekea mashindano hayo.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *