#Football #Sports

JUNIOR STARLETS WAREJEA

Timu ya taifa ya soka ya wanawake chipukizi Junior Starlets imerejea nchini kutoka Namibia ambako waliilaza wenyeji mabao 2-1 katika mashindano ya kuwania tiketi ya kufuzu mashindano ya FIFA U17 Women.

Kwa sasa chipukizi hao wanajiandaa kwa mechi ya marudiano dhidi ya wageni wao wikendi hii, na wameelekea moja kwa moja kwenye kambi ya mazoezi.

Namibia wanatarajiwa nchini hii leo huku wakisema kiwango cha Junior Starlets kinawazidi, ila watafanya kila wawezalo kubatilisha kichapo hicho.

Kocha mkuu wa Junior Starlets Mildred Cheche, anapanga kikosi chake upya kikiwajumuisha wanafunzi wa shule za upili baada ya wengi wa wachezaji walioshiriki dimba hilo mwaka wa 2024 kujiunga na kikosi cha U20.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *