#Local News

POLISI NAIROBI WAKATAA MAANDAMANO YALIYOPANGWA

Kamanda wa polisi jijini Nairobi Issa Mohamud amesema maandamano yaliyopangwa kufanyika Jumanne Aprili ishirini na moja hayatambuliwi kisheria kwa kuwa Hakuna taarifa rasmi iliyowasilishwa kwa Huduma ya Polisi nchini

Kauli hiyo inajiri kufuatia malalamishi ya Wakenya mtandaoni kuhusu kupanda kwa bei ya mafuta ambapo baadhi yao walikuwa wameitisha maandamano kupitia jumbe zilizosambaa katika mitandao ya kijamii

Akizungumza na wanahabari Mohamud amesema polisi hawapingi maandamano ya amani lakini amesisitiza kuwa sheria inahitaji waandalizi kutoa notisi ya siku kumi na nne kabla ya kufanyika kwa mkusanyiko wowote wa umma.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *