MBIO ZA UBINGWA ZAZIDI KUPAMBA MOTO LIGI KUU
Mbio za ubingwa wa ligi kuu ya Kenya zinaingia hatua muhimu mwishoni mwa wiki hii huku mechi za ushindani mkali zikitarajiwa kuamua mwelekeo wa msimamo wa ligi
AFC Leopards watachuana na mabingwa watetezi Kenya Police huku Gor Mahia wakipambana na Bandari walio katika kiwango kizuri hali inayoongeza presha kwa timu zinazowania ubingwa
Ushindi wa hivi karibuni wa Tusker dhidi ya Gor Mahia umefanya ushindani kuwa mkali zaidi huku tofauti ya alama ikiwa ndogo na kila timu ikihitaji ushindi ili kuendelea kuwa kwenye mbio za kutwaa taji la ligi kuu.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































