WATU KADHAA WAJERUHIWA WAKATI WA UCHAGUZI WA UDA

Baadhi ya wanachama na wagombezi wa viti mbali mbali wa chama cha UDA kaunti ya Busia wamejitokeza kushtumu ghasia zilizotokea wakati wa uchaguzi wa viongozi wa mashinani katika maeneobunge ya Funyula na Matayo siku ya jumamosi.
wakati wa uchaguzi huo watu kadhaa walijeruhiwa na kupelekea uchaguzi huo kusitishwa.
wakiongozwa na Stephen Buluma aliyegombea anawania wadhfa wa katibu wa kaunti wanachama hao wamewasuta baadhi ya viongozi na wagombezi kwa kuchangia vurugu hizo.
Madai ya wanachama wa vyama vingine kusimamia uchaguzi huo yameibuka badi ya kitaifa ya uchaguzi wa chama hicho ikitakiwa kujyachunguza.
Imetayarishwa na: Janice Marete
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































