#Football #Sports

BARONI ACHUKUA USUKANI LAZIO

Kilabu cha Lazio kimemteua Marco Baroni kama kocha wao mpya  kufuatia kuondoka kwa Igor Tudor baada ya miezi mitatu pekee katika wadhifa huo.

Mtaliano huyo mwenye umri wa miaka 60 ametia saini kandarasi ya miaka mingi.

Baroni anahamia Lazio baada ya msimu mmoja huko Verona, ambaye alimaliza katika nafasi ya 13 muhula uliopita, na hapo awali alifundisha Lecce kutoka 2021 hadi 2023.

Kazi ya Lazio iliachwa wazi Alhamisi iliyopita wakati Tudor aliripotiwa kuacha kazi kwani alikuwa na mzozo na mabosi wake kuhusu muundo wa kikosi cha sasa na malengo yake ya uhamisho.

Chini ya Tudor, ambaye alichukua mikoba ya Maurizio Sarri katikati ya mwezi Machi, Lazio walipata kichapo kimoja tu cha ligi, wakishinda mara tano na sare tatu.

Walimaliza katika nafasi ya saba kwenye Serie A na kupata nafasi ya mwisho ya kufuzu kwa Ligi ya Europa msimu ujao.

Imetayarishwa na Nelson Andati

BARONI ACHUKUA USUKANI LAZIO

ANGELA OKUTOYI AZIDI KUTAMBA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *