#Business

BAJETI YA MWAKA WA KIFEDHA 2024-2025 YASOMWA

Waziri wa fedha Njuguna ndung’u hapo jana aliwasilisha  bajeti  ya shilingi trilioni 3.9 ikiwa ni sawa na dola bilioni 30 za kimarekani kwa mwaka wa fedha wa 2024/2025,kwa bunge la kitaifa bajeti ambayo inalenga kuimarisha uchumi wa taifa.

Kulingana na Waziri wa fedha serikali inalenga kukuza uchumi baada ya kuimarika tena mwaka 2023 kwani kwa sasa uchumi wa taifa unaendelea kuimarika.

Aidha kuimarika kwa Uchumi kumechangiwa na kuongezeka kwa pato la taifa pale ambapo ilipanda asilimia 5.6 mwaka jana 2023, kutoka asilimia 4.9 mwaka 2022.Vile vile Ukuaji huo umechangiwa kwa kiasi kikubwa na ukuaji wa shughuli za kilimo, kutokana na kuimarika kwa hali ya hewa, na uwepo wa pembejeo za ruzuku.

Imetayarishwa na Maureen Amwayi

BAJETI YA MWAKA WA KIFEDHA 2024-2025 YASOMWA

MAHAKAMA IKO SALAMA

BAJETI YA MWAKA WA KIFEDHA 2024-2025 YASOMWA

WAKENYA WAPUMUA MIKONONI MWA EPRA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *