UPINZANI WADAI SERIKALI INAWAPUMBAZA
Ripoti ya kamati ya fedha na mipango katika bunge bunge la kitaifa kuhusu mswada wa fedha wa mwaka 2024-25 inaendelea kujadiliwa bungeni ambapo wabunge wanachambua mapendekezo ya kamati hiyo.
Haya yanajiri wakati ambapo wabunge wa upinzani wamepinga mswada huo, wakidai kwamba hatua ya serikali kuondoa baadhi ya mapendekezo ya ushuru kwa bidhaa kadhaa kwenye mswada huo inalenga kuwahadaa Wakenya.
Wakiongozwa na kinara wa walio wachache bungeni Opiyo Wandayi, wabunge hao wanashikilia mswada huo unaongeza mzigo kwa Mkenya.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































