PETER AGORO AELEKEA MAHAKAMANI KUTAKA BARAZA LA VIJANA LA KITAIFA KUFANYA UCHAGUZI
Ombi limewasilishwa kutaka kulazimisha Baraza la Kitaifa la Vijana kufanya uchaguzi wa wawakilishi wa vijana kama ilivyoainishwa katika katiba.
Katika ombi lake, Peter Agoro anahoji kuwa baraza hilo lilianzishwa ili kuwakilisha masilahi ya vijana nchini Kenya, kuwezesha ushiriki wao katika maendeleo ya kijamii, kiuchumi na kisiasa nchini.
Agoro anasema kuwa kushindwa kufanya uchaguzi unaohitajika kumesababisha ukosefu wa uwakilishi unaofaa kwa vijana
Imetayarishwa na Janice Marete
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































