KENYA INATARAJIWA KUAGIZA SUKARI ZAIDI KUTOKA NJE
Kenya inatarajiwa kurekodi ongezeko la uagizaji wa sukari kutoka nje, huku athari za kupiga marufuku usindikaji wa miwa ambayo haijakomaa zikianza,
Ripoti iliyotolewa na Kampuni ya Fitch Solutions BMI na Idara ya Kilimo ya Marekani inaonyesha kuwa nchi inapaswa kutarajia uzalishaji kupungua kwa asilimia 32.9 mwaka 2023/24 hadi tani elfu 530,000 kutoka tani 790,000 mwaka 2022/23.
Hii imechangiwa zaidi na marufuku ya uvunaji wa miwa ambayo ilitekelezwa mnamo Julai 2023.
Marufuku hiyo, iliyotekelezwa na Mamlaka ya Kilimo na Chakula ya Kenya mnamo Julai, iliruhusu tu viwanda kusindika miwa ikiwa vitathibitisha kuwa vina miwa iliyokomaa.
Marufuku hiyo ilitekelezwa kwani viwanda vimekuwa vikikosa miwa ya kusagwa, kwa sehemu kubwa kutokana na hali ya mvua ya wastani ambayo iliathiri Kenya kati ya 2020 na 2023
Kwa sababu hii, viwanda vingi vya kusaga sukari vilianza kugeukia kuponda miwa ambayo haijakomaa.
Uzalishaji wa sukari kwa wasagaji wa miwa wa Kenya ulipungua kwa asilimia 40 mwaka wa 2023 – chini ya miaka minne kutokana na uhaba wa miwa.
Jumla ya mahitaji ya sukari nchini inakadiriwa kuwa tani milioni 1.1 kila mwaka, tani 930,000 za sukari ya mezani na tani 170,000 za sukari ya viwandani.
Sekta hii ina uwezo wa kuzalisha zaidi ya tani milioni 1.47 za sukari ambayo ingeweza kukidhi mahitaji ya ndani na kutoa ziada endelevu kwa ajili ya kuuza nje ya nchi katika eneo la Comesa ambalo kwa ujumla ni eneo linaloagiza bidhaa kutoka nje.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































