SERIKALI YENYE MSINGI MPANA ITAFUNGUA UWEZO WA KENYA – RUTO
Rais William Ruto sasa anasema kuwa utawala wake mpya ulio na msingi mpana utafungua uwezo kamili wa nchi.
Akizungumza wakati wa kuapishwa kwa Makatibu 19 wa Baraza la Mawaziri walioidhinishwa, Ruto amesema Kenya imekuwa ikizuiliwa na ushindani wa kisiasa.
Ameongeza kusema kuwa wakati umefika ambapo maslahi ya nchi ni makubwa kuliko ya vyama vya siasa.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































