UMATI WAMUUA AFISA WA POLISI KWA KUJARIBU KUUA FAMILIA KWA MISHALE
Afisa mmoja wa polisi katika kituo cha Ng’ombeni Patrol Base kaunti ya Kwale ameuawa na kundi la vijana waliokuwa na hasira baada ya kujaribu kutumia silaha kushambulia familia moja eneo la Ziwani.
Kulingana na ripoti ya polisi Konstebo Titus Gaya anasemekana kuondoka kituoni bila kutambuliwa na kwenda kwenye nyumba ya Mwanaisha Ali mwendo wa saa 11:00 asubuhi.
Baada ya kupata njia ya kuingia kwenye nyumba hiyo, afisa huyo alijaribu kushambulia familia hiyo kwa kutumia pinde na mishale, na kusababisha hofu miongoni mwa jamaa za Ali, ambao walishangaa kupata mgeni kwenye majengo yao.
Muda mfupi baadaye, Mwanaisha alipiga nduru ambazo ziliwatahadharisha wakazi na jirani ambao walikimbilia nyumbani kwake na kumvamia afisa huyo hadi kufa.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































