WANJIGI AENDELEA ‘KULINDWA’ NA MAHAKAMA
Mahakama kuu imeongeza muda wa agizo la kuwazuia maafisa wa polisi dhidi ya kumakamata mfanyabaishara Jimi Wanjigi hadi tarehe 19 mwezi ujao.
Katika agizo hilo jipya, jaji Bahati Mwamuye ametoa uamuzi huo ingawa akadinda kutoa agizo la kuwazuia polisi kumfungulia mashtaka Wanjigi.
Kwa mujibu wa jaji huyo, ombi la Wanjigi mapema wiki hii linagusia tu masuala ya kukamatwa pekee, na kumpa siku 7 kuwasilisha ombo jipya.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































