MWANAMKE AZIKWA AKIWA HAI SHIMO LA MGODI WA DHAHABU LIKIPOROMOKA HUKO SIAYA
Mwanamke mwenye umri wa miaka 32 amefariki baada ya shimo la kuchimba dhahabu kuzamia na kumfunika akiwa hai katika kijiji cha Uradi, Kaunti ya Siaya.
Kulingana na Chifu Msaidizi wa eneo hilo Grace Otieno, mwanamke huyo kwa jina Rosemary Anyango alikuwa pamoja na wengine wanne alipokumbana na mauti.
Anasema kuwa wanawake hao walikuwa katika shughuli zao za kawaida za uchimbaji wakati shimoni lilipozama, na wanne kati yao walifanikiwa kutoroka wakiwa na majeraha madogo. Rosemary alikuwa amenaswa akiwa kwenye kina kirefu cha shimo.
Wakati wa kisa hicho, Brandon Omondi mwenye umri wa miaka 20 pia alipata majeraha alipokuwa akijaribu kuingia kwenye shimo lililoporomoka ili kumuokoa mwanamke aliyekuwa amefunikwa akiwa hai.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































