RUTO AONYA WACHAFUZI WA NAIROBI RIVER
Rais William Ruto ametangaza onyo kali dhidi ya kampuni na watu binafsi ambao wamekuwa wakitupa taka ndani Nairobi River, akisema watawajibishwa kisheria.
Akizungumza mtaani Korogocho jijini Nairobi wakati wa uzinduzi wa usafishaji wa mto huo, Rais amewaonya watakaokiuka agizo hilo kuwa tayari kuwajibikia mienendo yao.
Aidha, ameahidi kwamba nafasi 200000 za ajira zitabuniwa chini ya mradi huo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































