KENYA YAZINDUA ETA KURAHISISHA USAFIRI
Tangazo hilo limetolewa na Rais William Ruto wakati wa uzinduzi rasmi wa maonyesho ya utalii ya Magical Kenya uliofanyika katika Bustani ya Uhuru jijini Nairobi.
Ruto amesema hatua hiyo itawawezesha wasafiri kutoka nje ya uwanja wa ndege na kujionea wenyewe namna Kenya inavyovutia.
Wakati huohuo, Ruto amesema Kenya imetekeleza sera ya kutohitaji viza na hivyo kufanya iwe rahisi kwa Wakenya kuwakaribisha watu kutoka kila pembe ya dunia, wakiwemo watalii na wafanyabiashara.
Rais Ruto amesema anatambua wajibu muhimu unaotekelezwa na sekta ya utalii katika kubuni nafasi za ajira, kuendeleza miundombinu na kuilete a nchi hii fedha za kigeni.
Kufikia mwaka 2023, Kenya ilipokea zaidi ya watalii milioni mbili na kuiletea mapato ya shilingi bilioni 352.
Kulingana na Ruto, Kenya inalenga kuwavutia watalii milioni tano kila mwaka kufikia mwaka 2027.
Kwa upande wake, Waziri wa Utalii Rebecca Miano amesema juhudi kabambe zinafanywa ili kutumia sekta ya utalii kuchochea ukuaji uchumi nchini.
Imetayarishwa na Asami Mercy
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































