RUTO, GACHAGUA WAHIMIZWA KUPATANA
Baadhi ya wakazi wa kaunti ya Nyeri na Machakos wamehimiza uwiano baina ya Rais William Ruto na naibu wake Rigathi Gachagua ili kuruhusu utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Kulingana na wakazi hao, hoja ya kumbandua Gachagua imezua siasa za mapema ambazo wanahofia zitazuia utekelezwaji wa miradi hiyo.
Aidha, wamehimiza idara za serikali kutekeleza majukumu yake kikatiba bila kukubali shinikizo zozote.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































