TUPE MUDA TENA
Valencia leo wameomba mpambano wao wa raundi ya kwanza wa Copa del Rey na Parla Escuela uahirishwe tena kwa sababu ya mafuriko makubwa katika eneo hilo.
Takriban watu 217 walifariki, na wengine wengi bado hawajulikani walipo, baada ya dhoruba kali kupiga mashariki mwa Uhispania wiki iliyopita.
Mechi ya Valencia ya Copa del Rey awali ilipaswa kuchezwa wiki iliyopita lakini ilirudishwa nyuma hadi Novemba 6 na shirikisho la soka la Uhispania (RFEF).
Makocha na wachezaji kadhaa kutoka kwa timu za La Liga walipendekeza mechi zote zingeahirishwa wikendi badala ya mechi ya Valencia na Villarreal dhidi ya Rayo Vallecano pekee.
Kocha wa Atletico, Diego Simeone alisema “hakuna maana” kucheza mechi, wakati Hansi Flick wa Barcelona alisema kama ingekuwa juu yake angeghairi mzunguko mzima wa mechi.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































