KENHA YATANGAZA KUFUNGWA KWA MZUNGUKO WA BARABARA YA WAIYAKI WAY, SOUTHERN BYPASS
Shughuli za usafiri zinatarajiwa kutatizika kwenye mzunguko wa Waiyaki way, southern Bypass na ule wa Western Bypass.
Hii ni baada ya mamlaka ya kusimamia barabara kuu nchini KENHA kutangaza kufungwa kwa barabara hiyo eneo la Gitaru kwanzia tarehe 19 mwezi huu wa novemba hadi tarehe 19 mwezi decemba ili kupisha shughuli za ukarabati.
Mamlaka ya KENHA aidha imewataka madereva kutumia alama za barabarani ambazo zitawekwa na waadisi wake ili kuhakikisha usalama wa barabarani.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































