GAVANA WAIGURU APENDEKEZA KUBUNIWA KWA KITENGO MAALUM CHA KUKABILI MAUAJI YA WANAWAKE
Huku taifa la Kenya likisherehekea siku 16 za uhamasishaji kuhusu jinsia, Gavana wa Kirinyaga, Anne Waiguru, amezitaka mamlaka kuunda kitengo maalum cha polisi ndani ya Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) ili kushughulikia ongezeko la visa vya mauaji ya wanawake nchini.
Waiguru amesema kitengo hiki ndani ya muundo wa DCI kitasaidia kuchunguza na kuzuia mauaji ya wanawake yanayoendelea nchini.
Akitaja mauaji ya wanawake kama kielelezo kikuu cha ukatili dhidi ya wanawake, Gavana huyoameongeza kuwa suluhu la muda mrefu kwa mauaji ya wanawake na wasichana lazima lipatikane.
Kwa mujibu wake mashirika yote ya serikali lazima yachukue hatua haraka kuzuia ongezeko la mauaji hayo.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































